Newcastle United Yashinda Dhidi ya Arsenal
Newcastle United Yashinda Dhidi ya Arsenal | Newcastle United Yashinda kwa Mara ya Kwanza Ugenini Dhidi ya Arsenal, Yajiweka Hatiani kwa Fainali ya Carabao Cup
Newcastle United Yashinda Dhidi ya Arsenal
Newcastle United imefanikiwa kupata ushindi muhimu ugenini dhidi ya Arsenal kwa mara ya kwanza baada ya mechi 14, ikiwa ni hatua kubwa kuelekea kwenye fainali ya Kombe la Carabao (EFL Cup). Mchezo huo ulimalizika kwa ushindi wa 2-0 kwa Newcastle United, na sasa wamejipatia faida nzuri kuelekea mchezo wa marudiano.
Matokeo ya Mchezo:
- Arsenal 0-2 Newcastle United
⚽ 37’ Isak
⚽ 51’ Gordon
Ushindi huu unawaweka Newcastle kwenye nafasi nzuri ya kutinga fainali, huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kufanyika Februari 05, 2025, ambapo matokeo ya jumla yatatoa timu itakayokata tiketi ya kwenda fainali ya Carabao Cup.
Katika nusu fainali nyingine, Tottenham Hotspur itamenyana na Liverpool kesho Januari 08, 2025, kabla ya mchezo wa marudiano kufanyika Februari 06, 2025. Mchezo huu pia utatoa mshindi ambaye atakutana na Newcastle United kwenye fainali.
Pendekezo la Mhariri: