Pamba Jiji FC Kukata Mshahara Wachezaji Wanaochelewa Mazoezini
Pamba Jiji FC Kukata Mshahara Wachezaji Wanaochelewa Mazoezini | Klabu ya Pamba Jiji FC ya Tanzania imetangaza hatua mpya ya kuimarisha nidhamu ya wachezaji wake kwa kupitisha kanuni ya kukatwa shilingi 100,000 (laki moja) kwa siku kutoka kwenye mshahara wa mchezaji yeyote ambaye amechelewa mazoezini.
Pamba Jiji FC Kukata Mshahara Wachezaji Wanaochelewa Mazoezini
Hatua hii ni sehemu ya jitihada za klabu kuhakikisha wachezaji wanakuwa na nidhamu na ufanisi bora katika maandalizi ya mchezo wao.
Kando, Peter Rehett ameteuliwa kuwa Afisa Mkuu Mtendaji mpya (Mkurugenzi Mtendaji) wa Pamba Jiji FC na ataripoti moja kwa moja kwa Rais Bhiku Kotecha. Uteuzi huu unalenga kuimarisha uongozi wa klabu na kuhakikisha mikakati madhubuti inatekelezwa ili kufikia malengo ya mafanikio ya kimataifa na kikanda.
Mashabiki wa Pamba Jiji FC wanatarajiwa kuona mabadiliko makubwa katika uongozi na uchezaji wa klabu hiyo, na wadau wa soka wanatumai hatua hizo zitachangia mafanikio ya timu hiyo.
Pendekezo La Mhariri: