Polisi Tanzania Mbioni Kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara

Filed in Michezo Bongo by on January 12, 2025 0 Comments

Polisi Tanzania Mbioni Kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara | Polisi Tanzania wameendelea kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani, Ushirika Moshi, baada ya kuifunga Biashara United mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwishoni mwa wiki.

Polisi Tanzania Mbioni Kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Ofisa Habari wa Timu ya Polisi Tanzania, Frank Lukwaro alisema bado wana malengo ya kurejea kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara, huku akipongeza hamasa wanayoipata kutoka kwa mashabiki wao ambao wamejitokeza kwa wingi kuwatia moyo.

Amesema mipango yake kwa sasa ni kuhakikisha wanashinda michezo yao yote ili kuendelea kujiongezea pointi za kutosha ili mwisho wa ligi wawe kwenye nafasi nzuri.

Polisi Tanzania Mbioni Kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara

Polisi Tanzania Mbioni Kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara

Kwa upande wake kocha wa timu hiyo Benard Fabiano amebainisha kuwa ushindi huo ni chachu ya kufanya vizuri katika mechi zinazofuata huku nahodha wa timu hiyo Kassim Athuman amewapongeza wachezaji wenzake kwa kupambana na kupata pointi tatu Umoja.

Timu ya Polisi kwa sasa ipo nafasi ya kumi ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 15 ambazo tayari imemaliza mzunguko wa kwanza.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *