Ratiba ya Robo Fainali CAF Champions League na Kombe la Shirikisho 2025
Ratiba ya Robo Fainali CAF Champions League na Kombe la Shirikisho 2025 | Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetangaza tarehe za michuano ya robo fainali ya TotalEnergies CAF Champions League na Kombe la Shirikisho la CAF kwa mwaka 2025.
Ratiba ya Robo Fainali CAF Champions League na Kombe la Shirikisho 2025
Kwa mujibu wa ratiba, mechi za mkondo wa kwanza wa CAF Champions League zitafanyika tarehe 1 Aprili na 8 Aprili 2025, huku mechi za Kombe la Shirikisho zikichezwa tarehe 2 Aprili na 9 Aprili 2025.
Droo ya Nusu Fainali
Mbali na kuwapanga timu za robo fainali, droo hiyo pia itaamua wapinzani wa hatua ya nusu fainali kwa mashindano yote mawili. Mabingwa watetezi wa kila shindano pia watajumuishwa kwenye droo hiyo:
- Al Ahly SC (Misri) – Mabingwa wa CAF Champions League
- Zamalek SC (Misri) – Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la CAF

Ratiba ya Robo Fainali CAF Champions League na Kombe la Shirikisho 2025
Timu Zilizofuzu Robo Fainali
CAF Champions League 2025
- Al Ahly SC (Misri)
- Al Hilal (Sudan)
- AS FAR (Morocco)
- Espérance Sportive de Tunis (Tunisia)
- Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
- Orlando Pirates (Afrika Kusini)
- Pyramids (Misri)
- MC Alger (Algeria)
Kombe la Shirikisho la CAF 2025
- Zamalek SC (Misri)
- Asec Mimosas (Cote d’Ivoire)
- Al Masry (Misri)
- CS Constantine (Algeria)
- RS Berkane (Morocco)
- Simba SC (Tanzania)
- Stellenbosch FC (Afrika Kusini)
- USM Alger (Algeria)
Michuano hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku mashabiki wakisubiri kuona nani ataibuka na ubingwa wa msimu wa 2025. Endelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusu ratiba rasmi na matokeo ya droo.
Pendekezo La Mhariri: