Robertinho Aomba Nafasi ya Kuifundisha Timu ya Taifa ya Rwanda
Robertinho Aomba Nafasi ya Kuifundisha Timu ya Taifa ya Rwanda | KOCHA Mbrazil, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’ ametangaza kutamani kupata nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya Rwanda, huku akieleza dhamira yake ya kulisaidia taifa hilo kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Robertinho Aomba Nafasi ya Kuifundisha Timu ya Taifa ya Rwanda
Robertinho ni miongoni mwa makocha wa Brazil waliopata mafanikio nje ya nchi yao, wakiwa na historia ya kutwaa mataji kadhaa wakiwa na klabu tofauti barani Afrika. Hii si mara yake ya kwanza kufanya kazi nchini Rwanda, kwani mwaka wa 2019 aliifundisha Gikundiro (Rayon Sports FC) na kuwa na wakati mzuri na timu hiyo.

Robertinho Aomba Nafasi ya Kuifundisha Timu ya Taifa ya Rwanda
Kujitolea kwake kwa timu ya taifa ya Rwanda
Katika mahojiano yake, Robertinho amebainisha kuwa Rwanda ina wachezaji wengi chipukizi wenye vipaji, na anaamini akipewa nafasi ya kuifundisha timu hiyo anaweza kuiboresha na kuhakikisha inafikia viwango vya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia.
FERWAFA inatafuta kocha mpya
SHIRIKISHO la Soka la Rwanda (FERWAFA) limeanza harakati za kusaka kocha mpya wa timu ya taifa, baada ya kumtimua Torsten Frank Spittler. Robertinho ameweka wazi kuwa ana nia ya kuchukua kibarua hicho huku mashabiki wa soka wakisubiri kuona iwapo atapewa nafasi ya kuwaongoza Amavubi katika kampeni zao za kufuzu kwa michuano mikubwa ya kimataifa.
Pendekezo La Mhariri: