Simba Kurejea Mazoezini Kujiandaa Dhidi ya Kilimanjaro Wonders
Simba Kurejea Mazoezini Kujiandaa Dhidi ya Kilimanjaro Wonders | Baada ya mapumziko ya siku nne wachezaji wa Simba SC watarejea mazoezini Ijumaa tarehe 24 Januari 2025 kujiandaa na mchezo wao wa FA dhidi ya Kilimanjaro Wonders utakaopigwa Jumapili ya tarehe 26 Januari 2025.
Simba Kurejea Mazoezini Kujiandaa Dhidi ya Kilimanjaro Wonders
Klabu inajiandaa kuendeleza rekodi yake nzuri. katika mashindano ya ndani na inalenga kupata matokeo mazuri kwenye Kombe la FA.
Kwa wachezaji, mapumziko haya yatakuwa muhimu ili kurejesha nguvu na kujiandaa kisaikolojia kwa changamoto iliyo mbele yao. Simba SC ambayo imekuwa na matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu, inahitaji ushindi katika mchezo huu ili kuweka mazingira mazuri ya kiushindani kwenye michuano ya FA na kuongeza ari ya wachezaji kuelekea mechi zijazo.
Mchezo wa FA dhidi ya Kilimanjaro Wonders unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwani Kilimanjaro Wonders nao wana timu imara na inahitaji kupata matokeo mazuri kwenye michuano hiyo.
WACHEZAJI wa Simba SC wanatarajiwa kufanya mazoezi makali ili kuhakikisha wanajiandaa vya kutosha kuelekea mchezo huo muhimu na kufanya kazi pamoja chini ya uongozi wa kocha wao.
Pendekezo La Mhariri: