Simba na Rekodi ya Kufungwa Magoli Machache Ligi Kuu
Simba na Rekodi ya Kufungwa Magoli Machache Ligi Kuu | Walinda mlango bora NBC, Rekodi za Ligi Kuu NBC, Timu zilizofungwa mabao machache Tanzania.
Simba na Rekodi ya Kufungwa Magoli Machache Ligi Kuu
Timu ya Simba SC imeweka rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi hadi sasa katika Ligi Kuu ya NBC, ikiwa imefungwa mabao matano (5) pekee. Simba inashikilia nafasi ya kwanza kwenye orodha ya timu zilizofungwa mabao machache, ikifuatiwa na wapinzani wao wa jadi Yanga SC ambao wamefungwa mabao sita (6).
Orodha ya Timu Zilizofungwa Mabao Machache Ligi Kuu NBC:
- Simba SC – Mabao 5
- Yanga SC – Mabao 6
- Azam FC – Mabao 8
- Singida BS – Mabao 11
- JKT Tanzania – Mabao 12
Walinda Mlango Bora wa Ligi Kuu NBC
Walinda mlango wanne wanaongoza kwa kudaka mechi zote za timu zao hadi sasa. Wanafanya kazi kubwa kuhakikisha timu zao zinapata matokeo bora:
- Moussa Pinpin Camara (Simba SC): Amecheza mechi 15.
- Metacha Mnata (Singida BS): Amecheza mechi 16.
- Ramadhani Chalamanda (JKT Tanzania): Amecheza mechi 16.
- Yona Amosi (Prisons FC): Amecheza mechi 16.
Simba SC imeonyesha uimara wa safu ya ulinzi na uwezo wa walinda mlango wao, hatua inayowaweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu NBC msimu huu.
Pendekezo la Mhariri: