Simba na Yanga Katika Viwango CAF vya Ubora wa Vilabu Afrika

Filed in Michezo Bongo by on January 23, 2025 0 Comments

Simba na Yanga Katika Viwango CAF vya Ubora wa Vilabu Afrika | Baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika CAF kwa mara nyingine, Simba SC imepanda hadi nafasi ya sita kwenye viwango vya ubora wa vilabu barani Afrika na kuiondoa timu ya RS Berkane ya Morocco kutoka nafasi ya sita hadi ya saba.

Haya ni mafanikio makubwa kwa klabu ya Simba SC kutokana na mafanikio yake katika mashindano ya kimataifa, ikiwa na pointi 38.

Kwa upande mwingine, Yanga SC nayo imepiga hatua kubwa, ikipanda hadi nafasi ya kumi kutoka ya 13, na sasa iko juu zaidi ya klabu kubwa kama Raja Casablanca, TP Mazembe na Petro AtlΓ©tico. Yanga SC ina pointi 34 katika viwango hivi vya ubora.

Simba na Yanga Katika Viwango CAF vya Ubora wa Vilabu Afrika

Simba na Yanga Katika Viwango CAF vya Ubora wa Vilabu Afrika

Simba na Yanga Katika Viwango CAF vya Ubora wa Vilabu Afrika

Orodha Kamili ya Timu 10 Bora Afrika

  1. Al Ahly β€” 73 points πŸ‡ͺπŸ‡¬
  2. Esperance Sportive de Tunis β€” 57 points πŸ‡ΉπŸ‡³
  3. Mamelodi Sundowns β€” 52 points πŸ‡ΏπŸ‡¦
  4. Zamalek SC β€” 42 points πŸ‡ͺπŸ‡¬
  5. Wydad Athletic Club β€” 39 points πŸ‡²πŸ‡¦
  6. Simba SC β€” 38 points πŸ‡ΉπŸ‡Ώ
  7. RS Berkane β€” 37 points πŸ‡²πŸ‡¦
  8. USM Alger β€” 37 points πŸ‡©πŸ‡Ώ
  9. CR Belouizdad β€” 36 points πŸ‡©πŸ‡Ώ
  10. Young Africans β€” 34 points πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Simba SC na Yanga SC wakiwa kileleni mwa soka la Afrika

Simba SC na Yanga SC zinazidi kudhihirisha nguvu na mafanikio katika mashindano ya kimataifa, na kupanda kwao kileleni mwa ligi kunaonyesha kuwa soka la Tanzania linapiga hatua. Simba SC kwa kutinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho, na Yanga SC, kwa kuendelea kutinga kwenye Ligi ya Mabingwa, ni dalili tosha ya maendeleo ya soka la Tanzania.

Klabu hizi mbili za Tanzania zinaonyesha kwa vitendo jinsi zinavyochuana kuwania nafasi za juu katika viwango vya ubora wa Afrika na mashabiki wa soka nchini wana matumaini makubwa ya kuendelea kufanikiwa katika michuano ijayo/Simba na Yanga Katika Viwango CAF vya Ubora wa Vilabu Afrika.

Pendekezo la Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *