Simba Yafuzu Robo Fainali ya CAF Kombe la Shirikisho Afrika
Simba Yafuzu Robo Fainali ya CAF Kombe la Shirikisho Afrika | Yakutana na Mmoja kati ya Stellenbosch, Asec Mimosas, au Al Masry.
Baada ya kumaliza kileleni mwa Kundi A, wawakilishi wa Tanzania, Simba SC, wamefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Katika hatua hii, Simba SC itakutana na mmoja kati ya washindi wa pili wa makundi B, C, na D.
Simba Yafuzu Robo Fainali ya CAF Kombe la Shirikisho Afrika
Timu ambazo zimejihakikishia nafasi ya kushiriki robo fainali ni Stellenbosch ya Afrika Kusini, Asec Mimosas ya Ivory Coast, na Al Masry ya Misri.
Timu zilizofuzu robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ni kama ifuatavyo:
- Kundi A:
- 🇹🇿 Simba SC (Tanzania)
- 🇩🇿 CS Constantine (Algeria)
- Kundi B:
- 🇲🇦 RS Berkane (Morocco)
- 🇿🇦 Stellenbosch (Afrika Kusini)
- Kundi C:
- 🇩🇿 USM Alger (Algeria)
- 🇨🇮 Asec Mimosas (Ivory Coast)
- Kundi D:
- 🇪🇬 Zamalek (Misri)
- 🇪🇬 Al Masry (Misri)
Simba SC, wakiwa na alama 13, walimaliza kileleni kwa ufanisi mkubwa, wakifuatiliwa na CS Constantine ambao pia walijizolea alama 10. Hii inamaanisha kuwa Simba SC sasa itakutana na mmoja kati ya Stellenbosch, Asec Mimosas, au Al Masry katika robo fainali, ambapo watakuwa na lengo la kutinga nusu fainali ya mashindano haya muhimu barani Afrika.