Simba Yaichapa Namungo 3-0, Camara Afikia Rekodi ya Clean Sheets

Filed in Michezo Bongo by on February 19, 2025 0 Comments

Simba Yaichapa Namungo 3-0 | Simba SC Yatamba Ruangwa huku Camara Afikia Rekodi ya Clean Sheets 15 | Simba SC imepata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Ushindi huo umewafanya Wekundu wa Msimbazi kupata pointi tatu muhimu wakiwa ugenini, huku mechi hiyo ikipigwa penalti tatu, mbili kati ya hizo zikifungwa na Ahoua moja Ateba aliyoikosa.

Simba Yaichapa Namungo 3-0, Camara Afikia Rekodi ya Clean Sheets

Simba SC walianza kwa kasi na kupata penalti mwishoni mwa kipindi cha kwanza, ambapo Ahoua alifunga bao kali katika dakika ya 45+4. Baada ya mapumziko, Namungo FC walijaribu kurejea uwanjani, lakini Simba waliendeleza ubora wao wa kipindi cha kwanza. Penati ya pili ilitolewa katika dakika ya 72 na tena Ahoua hakuwa na papara na kutumbukiza mpira kimyani, akifunga kwa mara ya pili.

Simba Yaichapa Namungo 3-0, Camara Afikia Rekodi ya Clean Sheets

Simba Yaichapa Namungo 3-0, Camara Afikia Rekodi ya Clean Sheets

Katika dakika za nyongeza, Steven Mukwala aliifungia Simba SC bao la tatu dakika ya 90+1, na kuipa ushindi mnono kikosi cha kocha Fadlu.

Camara anaweka rekodi safi ya clean sheet

Mlinda mlango wa Simba SC, Moussa Camara ameendelea kung’ara msimu huu baada ya kufikisha michezo 15 bila kufungwa, rekodi ambayo iliwekwa msimu uliopita na Ley Matampi wa Coastal Union. Camara amekuwa mchezaji muhimu kwenye safu ya ulinzi ya Simba na rekodi yake inaonyesha uthabiti wake langoni msimu huu.

🏆 FT: Namungo FC 0-3 Simba SC
45+4’ Kouassi Attohoula Ahoua (P)
72’ Kouassi Attohoula Ahoua (P)
90+1’ Steven Mukwala

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *