Singida Black Stars Yathibitisha Kumsajili Serge Pokou
Singida Black Stars Yathibitisha Kumsajili Serge Pokou kutoka Al Hilal. Klabu ya Singida Black Stars imethibitisha rasmi kukamilisha usajili wa winga kutoka Ivory Coast, Serge Pokou, mwenye umri wa miaka 24, kutoka klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan.
Singida Black Stars Yathibitisha Kumsajili Serge Pokou
Pokou, ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Asec Mimosas ya Ivory Coast kwa kipindi cha miaka mitano, amehamia Singida Black Stars baada ya kuwa na msimu mmoja katika klabu ya Al Hilal.
Singida Black Stars wamethibitisha usajili huu kupitia mitandao yao rasmi ya kijamii, wakionesha furaha yao kumkaribisha nyota huyo mwenye talanta, ambaye anatarajiwa kuleta mchango mkubwa kwa timu hiyo katika michuano ya ndani na kimataifa.
Serge Pokou alionyesha kiwango cha juu akiwa Asec Mimosas, ambapo alikisaidia kikosi hicho kwa ufanisi katika michuano ya ligi ya Ivory Coast na michuano ya kimataifa. Baada ya kutimkia Al Hilal msimu uliopita, sasa atajiunga na Singida Black Stars, ambayo imeendelea kufanya usajili bora kwa lengo la kuimarisha kikosi chao kwa msimu huu.
Pendekezo La Mhariri: