Sowah Aifungia Singida Black Stars Bao la Ushindi Dhidi ya JKT Tanzania
Sowah Aifungia Singida Black Stars Bao la Ushindi Dhidi ya JKT Tanzania | Jonathan Sowah akiifungia Singida Black Stars bao la ushindi dhidi ya JKT Tanzania.
Sowah Aifungia Singida Black Stars Bao la Ushindi Dhidi ya JKT Tanzania
Timu ya Singida Black Stars imefanikiwa kutwaa pointi tatu muhimu kutoka kwa JKT Tanzania baada ya Jonathan Sowah kufunga bao la ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo. Bao la Sowah alilofunga dakika ya 52, likiwa ni bao lake la pili msimu huu na kuisaidia Singida Black Stars kushinda 1-0.
JKT Tanzania ilikuwa na matumaini ya kuendeleza kasi yake baada ya kutoka na pointi moja dhidi ya Yanga SC katika mechi iliyopita, lakini hawakuweza kudhibiti kasi ya Singida Black Stars. Hata hivyo, licha ya kushindwa kupata ushindi huo, JKT Tanzania bado inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 19. Kwa upande mwingine, Singida Black Stars wameendelea kushika nafasi ya nne wakiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 19.

Sowah Aifungia Singida Black Stars Bao la Ushindi Dhidi ya JKT Tanzania
Mechi hii ilionyesha jinsi Jonathan Sowah alivyo muhimu kwa timu yake, huku pia akionyesha ubora wake katika michuano ya ligi kuu Tanzania bara.
Pendekezo La Mhariri: