Taifa Stars Yapangwa Kundi B Kombe la Mataifa Afrika CHAN 2025
Taifa Stars Yapangwa Kundi B Kombe la Mataifa Afrika CHAN 2025 | Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepangwa katika kundi B kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) 2025, ambayo itafanyika nchini Tanzania, Kenya, na Uganda kuanzia Agosti 2025.
Katika kundi hili, Taifa Stars itachuana na timu za Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Droo ya michuano ya CHAN 2025 ilifanyika leo nchini Kenya na imetoa makundi manne yenye timu 16, ambapo kila kundi linaundwa na timu tano.
Taifa Stars Yapangwa Kundi B Kombe la Mataifa Afrika CHAN 2025
Huu ni ushindani mkubwa kwa Tanzania, kwani timu zote zilizopangwa katika kundi lao zina historia nzuri katika michuano ya kimataifa, hivyo Taifa Stars itahitaji maandalizi bora ili kutamba kwenye mashindano haya.
Makundi ya CHAN 2025:
- Kundi A: Kenya, Morocco, Angola, DR Congo, Zambia
- Kundi B: Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, Central Africa.
- Kundi C: Uganda, Niger, Guinea, Q2, Q1
- Kundi D: Senegal, Congo, Sudan, Nigeria
Mataifa ya Q1 na Q2 yatatolewa baadaye kutoka kwa mataifa saba, ambayo ni Algeria, Afrika Kusini, Malawi, Gabon, na mengine.
Pendekezo La Mhariri: