Tanzania na Uganda Zafuzu AFCON U-17 2025
Tanzania na Uganda Zafuzu AFCON U-17 2025 | Ushindi Mkubwa Katika Nusu Fainali CECAFA. Tanzania na Uganda zimefanikiwa kufuzu kuwakilisha Kanda ya CECAFA katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (AFCON U-17) mwaka 2025, ambayo itafanyika nchini Morocco.
Tanzania na Uganda Zafuzu AFCON U-17 2025
Mafanikio haya yamepatikana baada ya ushindi mkubwa katika mechi za nusu fainali zilizochezwa Jumanne, Desemba 24, 2024, kwenye Uwanja wa Nakivubo Hamz mjini Kampala, Uganda.
Tanzania Yatinga Fainali kwa Ushindi wa Mabao 4-0
Timu ya Taifa ya Tanzania ilipata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Sudan Kusini. Katika kipindi cha kwanza, Tanzania ilionyesha uwezo wa hali ya juu, ikifunga mabao matatu kupitia Hussein Mbegu, Ng’habi Zamu, na Abel Josiah Samson. Sudan Kusini ilijaribu kupambana baada ya mapumziko, lakini ilishindwa kupenya safu ya ulinzi ya Tanzania.
Mchezaji wa akiba Juma Abushiri aliongeza bao la nne kwa Tanzania dakika ya 52, akihitimisha mchezo huo kwa ushindi wa kishindo. Sudan Kusini ilipewa penalti dakika ya 67 baada ya beki wa Tanzania Idrisa Kilendewo kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari, lakini kipa wa Tanzania, Abrahman Masssoro, aliokoa penalti iliyopigwa na Lazarus Peter George Laku.
Uganda Yafuzu kwa Ushindi Dhidi ya Somalia
Katika nusu fainali nyingine, Uganda iliwashinda Somalia kwa mabao 4-1. Ushindi huo uliipa Uganda tiketi ya kuingia fainali na nafasi ya kushiriki AFCON U-17 2025.
Mechi Zinazofuata
Sudan Kusini na Somalia zitakutana kuwania nafasi ya tatu, huku Tanzania na Uganda zikitarajiwa kupambana katika mechi ya fainali ya mashindano ya CECAFA U-17. Mechi hizi zitachezwa Desemba 27, 2024, kwenye uwanja huohuo wa Nakivubo Hamz/Tanzania na Uganda Zafuzu AFCON U-17 2025.
Tanzania na Uganda sasa zinajiandaa kwa michuano ya AFCON U-17 2025, ambapo zitakuwa wawakilishi wa Kanda ya CECAFA. Ushindi wao katika nusu fainali unaashiria kiwango cha juu cha maendeleo ya soka la vijana katika ukanda huu, huku timu hizo zikiwa na matumaini makubwa ya kufanikisha ushindani wa hali ya juu nchini Morocco.
Pendekezo La Mhariri: