Uganda Yaibuka Mabingwa wa AFCON CECAFA U-17 2024
Uganda Yaibuka Mabingwa wa AFCON CECAFA U-17 2024 | Timu ya vijana ya Uganda U-17 imeonyesha uwezo mkubwa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania katika fainali ya michuano ya kufuzu kwa AFCON CECAFA U-17 2024.
Uganda Yaibuka Mabingwa wa AFCON CECAFA U-17 2024
Mchezo huo wa kusisimua ulifanyika mbele ya mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya wachezaji chipukizi/Uganda Yaibuka Mabingwa wa AFCON CECAFA U-17 2024.
Tanzania, licha ya kuonyesha upinzani mkali, walifanikiwa kufunga bao moja ambalo halikutosha kuwazuia vijana wa Uganda kuibuka na ushindi. Uganda ilionyesha nidhamu ya hali ya juu uwanjani na kutumia nafasi walizopata kwa ufanisi, jambo lililowahakikishia ushindi wa kihistoria.
Hongera Uganda
Kwa ushindi huu, Uganda imejihakikishia nafasi ya heshima katika michuano ya AFCON U-17 itakayofanyika mwaka 2024. Mafanikio haya yanasisitiza maendeleo ya soka la vijana nchini Uganda, huku wakiwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine za ukanda wa CECAFA.
Pamoja na kupoteza fainali, Tanzania imepongezwa kwa juhudi zao na kwa kufikia hatua ya mwisho ya mashindano haya makubwa. Ni dalili nzuri kwamba soka la vijana linaendelea kukua nchini Tanzania.
Tuzo Ilizo Pata kwenye Michuano hii ya Kufuzu AFCON U17
Timu ya Taifa ya wanaume U17 @SerengetiBoys imechua Tuzo ya mchezo wa kiungwana (Fair Play) katika michuano ya kufuzu AFCON U17 2025 Kanda ya CECAFA. @SerengetiBoys pic.twitter.com/UaeXsu7SgJ
— TFF TANZANIA (@Tanfootball) December 27, 2024
- Timu ya Taifa ya wanaume U17 Serengeti Boys imechua Tuzo ya mchezo wa kiungwana (Fair Play) katika michuano ya kufuzu AFCON U17 2025 Kanda ya CECAFA.
- Golikipa wa Timu ya Taifa ya wanaume U17 Serengeti Boys Abrahman Vuai amekua kipa bora wa michuano ya kufuzu AFCON U17 2025 Kanda ya CECAFA.
Michuano ya AFCON CECAFA U-17 imekuwa jukwaa muhimu kwa wachezaji chipukizi kuonyesha vipaji vyao na kuandaa safari za mafanikio katika soka la kimataifa. Hongera Uganda kwa kuwa mabingwa wapya wa CECAFA U-17 2024!
Pendekezo La Mhariri: