Yanga Yajikita Kileleni Baada ya Kuichapa KMC 6-1

Filed in Michezo Bongo by on February 14, 2025 0 Comments

Yanga Yajikita Kileleni Baada ya Kuichapa KMC 6-1 | Hatua hiyo ilihitimishwa kwenye Uwanja wa KMC Complex ambapo Klabu ya Yanga SC imeendelea na Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya wenyeji KMC FC. Ushindi huo unaifanya Wananchi kufikisha pointi 49 baada ya kucheza mechi 19, wakiongoza msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi mbili na Simba SC, ambao wana mchezo mkononi.

Yanga Yajikita Kileleni Baada ya Kuichapa KMC 6-1

KMC FC 1-6 Yanga SC

⚽ 11’ – Prince Dube
⚽ 18’ – Stephane Aziz Ki (P)
⚽ 49’ – Stephane Aziz Ki
⚽ 52’ – Redemptus
⚽ 56’ – Stephane Aziz Ki (P)
⚽ 90’ – Maxi
⚽ 90+4’ – Mwenda

Katika msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC wamefunga jumla ya mabao 48 na kuruhusu mabao 8 pekee baada ya mechi 19, hali inayodhihirisha nguvu zao kwenye safu ya ushambuliaji na ulinzi.

Yanga Yajikita Kileleni Baada ya Kuichapa KMC 6-1

Yanga Yajikita Kileleni Baada ya Kuichapa KMC 6-1

Prince Dube akiendelea kung’ara

MSHAMBULIAJI Prince Dube ameendelea kuwa mchezaji tegemeo wa Yanga SC baada ya kufunga bao moja na kutoa asisti moja katika mechi hii. Kwa sasa Dube ana jumla ya mabao 8 na asisti 7, akiwa ameweka rekodi ya kuhusika katika mabao 15 ya Yanga SC msimu huu, zaidi ya mchezaji yeyote kwenye kikosi hicho.

Matokeo Mengine ya Ligi Kuu ya NBC

  • Tanzania Prisons 0-1 Namungo FC
  • Kagera Sugar 3-0 Fountain Gate

Kwa ushindi huu, Yanga SC imeendelea kuweka presha kwa Simba SC katika mbio za ubingwa, huku wakitarajia kuendeleza rekodi yao nzuri kwenye michezo ijayo. Mashabiki wa Wananchi wana matumaini makubwa ya kutetea ubingwa wao msimu huu/Yanga Yajikita Kileleni Baada ya Kuichapa KMC 6-1.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *