Yanga Yaomboleza Kifo cha Baba wa Chadrack Boka
Yanga Yaomboleza Kifo cha Baba wa Chadrack Boka | Beki wa kushoto wa klabu ya Yanga, Chadrack Boka (25) raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), amepata pigo kubwa kufuatia kifo cha baba yake mzazi kilichotokea Januari 11, 2025 nyumbani kwake Kinshasa, DRC. . Kifo cha baba yake kimeacha machungu makubwa kwa familia ya Boka na wapenzi wa michezo hasa mashabiki wa klabu ya Yanga ambayo Boka ni mchezaji wake.
Yanga Yaomboleza Kifo cha Baba wa Chadrack Boka
Klabu ya Yanga kupitia uongozi wake imetuma salamu za rambirambi kwa Boka na familia yake kuwaunga mkono katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Uongozi wa Yanga umeonyesha mshikamano wake na mchezaji wake huyo ukisema upo kwa Boka na familia yake huku ukiomba uvumilivu na matumaini katika kipindi hiki cha machungu.
Boka aliyejiunga na Yanga baada ya kuonesha kiwango kizuri katika ligi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akiwa na FC Saint Loi Lupopo, ameendelea kuonyesha viwango vya juu tangu ajiunge na timu hiyo. Kwa sasa anasubiri kuunganishwa na wachezaji wenzake kufuatia tukio hili la kusikitisha.
Klabu ya Yanga na mashabiki wake wameeleza matumaini yao kuwa Mungu atampa Boka na familia yake nguvu ya kuvumilia maumivu hayo na wametuma maombi ya kuiombea roho ya marehemu baba yake mzazi apumzike kwa amani.
Wakati huo huo mashabiki na wapenzi wa soka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania wamesikitishwa na msiba huo mkubwa na wameonyesha upendo na mshikamano wao kwa Boka na familia yake katika kipindi hiki cha majonzi.
Pendekezo La Mhariri: