Yanga Yasitisha Usajili wa Beki Laurian Makame

Filed in Michezo Bongo by on December 31, 2024 0 Comments

Yanga Yasitisha Usajili wa Beki Laurian Makame | Klabu ya Yanga SC imeamua kusitisha mpango wa kumsajili beki Laurian Makame kutoka Fountain Gate, licha ya kuwa awali walishakubaliana kila kitu, ikiwemo ada ya usajili.

Yanga Yasitisha Usajili wa Beki Laurian Makame

Taarifa zinaeleza kuwa hatua hiyo ilifikiwa baada ya kocha wa Yanga SC, Nasreddine Nabi Ramovic, kumtazama Laurian Makame kwenye mchezo wa Fountain Gate dhidi ya Azam FC. Baada ya tathmini yake ya kiufundi, Ramovic alitoa ushauri kwa uongozi wa Yanga kusitisha mpango wa usajili wa beki huyo.

Hatua hii inadhihirisha jinsi Yanga SC inavyotoa kipaumbele kwa tathmini ya kiufundi kabla ya kukamilisha usajili wa wachezaji, ikilenga kuwa na kikosi bora chenye ushindani wa hali ya juu.

Yanga Yasitisha Usajili wa Beki Laurian Makame

Yanga Yasitisha Usajili wa Beki Laurian Makame

Uamuzi huu unaweza kuwa pigo kwa Laurian Makame ambaye alikuwa akitarajia kujiunga na moja ya klabu kubwa nchini. Hata hivyo, unaonyesha dhamira ya Yanga kuhakikisha wanachagua wachezaji wanaoendana na mahitaji ya kikosi chao kwa misingi ya kitaalamu.

Pendekezo la Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *