Yao, Nzengeli, Andambwile Kuikosa Al Hilal
Yao, Nzengeli, Andambwile Kuikosa Al Hilal | Wachezaji watakaokosekana dhidi ya Al Hilal tarehe 12 January 2025.
Afisa Habari Mkuu wa timu ya Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa wachezaji watatu muhimu wa timu yake, Maxi Nzengeli, Kouassi Attohoula, na Aziz Andambwile hawatacheza katika mchezo ujao dhidi ya Al Hilal.
Yao, Nzengeli, Andambwile Kuikosa Al Hilal
Hii inatokana na ushauri wa jopo la madaktari wa timu, ambao wameeleza kwamba afya zao bado hazijaimarika. Kutokana na hali hiyo, wachezaji hao wataendelea kutibiwa na hawatatumika kwenye mechi hiyo muhimu.
“Kutokana na ushauri ambao tumepatiwa na jopo letu la madaktari ni kuwa wachezaji wetu watatu Maxi Nzengeli, Kouassi Attohoula pamoja na Aziz Andambwile afya zao hazijaimarika”. Amesema Ali Kamwe
Timu inajiandaa kwa changamoto kubwa dhidi ya Al Hilal, lakini ni wazi kuwa kukosekana kwa wachezaji hawa kutaleta changamoto katika mikakati ya mchezo. Wakati huu, kamati ya mafunzo inatafuta mbinu za kuboresha utendaji wa timu bila ya wachezaji hawa muhimu.
Pendekezo la Mhariri: