Zanzibar Heroes Yatinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2025
Zanzibar Heroes Yatinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2025
Zanzibar Heroes Yatinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2025 | Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2025 imeendelea kwa msisimko, huku Zanzibar Heroes ikijihakikishia nafasi ya kucheza fainali baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Harambee Stars ya Kenya.
Mchezo huo wa nusu fainali, uliofanyika Januari 10, 2025, ulikuwa wa vuta nikuvute na ulishuhudia idadi kubwa ya kadi zikionyeshwa na mwamuzi.
Matokeo ya Mchezo
- FT: Kenya 0-1 Zanzibar Heroes
- ⚽ Bao: Ali Juma ‘Inzangi’ dakika ya 90+4
#MapinduziCup2025 Goli pekee lililowapa Zanzibar tiketi ya kucheza fainali… mfungaji ni ‘super-sub’, Ali Khatibu Inzagi…Dakika za jioooooooooooooni.
FT: Kenya 0-1 Zanzibar
Tukutane Januari 13 LIVE #AzamSports1HD#MapinduziCup #MapinduziCup2025 #MapinduziCupPemba… pic.twitter.com/qPa5ybjG5v
— Azam TV (@azamtvtz) January 10, 2025
Bao hilo la dakika za majeruhi lilifungwa na Ali Juma maarufu kama ‘Inzangi,’ ambaye alitokea shujaa wa Zanzibar Heroes kwa kuipa timu yake tiketi ya fainali.
Mchezo huu ulisimama kama mmoja wa mechi zenye ushindani mkubwa, huku mwamuzi akitoa kadi 10 kwa wachezaji wa timu zote mbili. Kadi nyekundu mbili zilitolewa pamoja na kadi za njano 8, hali iliyodhihirisha ukali wa pambano hilo.
Ratiba ya Fainali
Zanzibar Heroes sasa itaingia fainali kukutana na Burkina Faso, timu ambayo pia imeonyesha uwezo mkubwa katika michuano hii. Mchezo wa fainali unatarajiwa kupigwa Januari 13, 2025, kwenye Uwanja wa Gombani, na unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa soka kutoka kila kona ya Zanzibar na kwingineko.
Pendekezo La Mhariri: