Zanzibar Heroes Yatwaa Kombe la Mapinduzi 2025
Zanzibar Heroes Yatwaa Kombe la Mapinduzi 2025 kwa Ushindi wa 2-1 Dhidi ya Burkina Faso
Zanzibar Heroes Yatwaa Kombe la Mapinduzi 2025
Zanzibar Heroes imeibuka mabingwa wa Kombe la Mapinduzi 2025 baada ya kuichapa Burkina Faso kwa mabao 2-1 katika fainali ya kusisimua iliyopigwa katika dimba la Gombani, Zanzibar.
Mchezo huo ulianza kwa kasi, na Ibrahim Hamad Hilika aliifungia Zanzibar Heroes bao la kuongoza dakika ya 41, akionyesha ubora wake mbele ya lango la Burkina Faso. Timu ya Burkina Faso ilijitahidi kurejesha hali ya mchezo, na dakika ya 70, Aboubakar Traore alifunga bao la kusawazisha, akileta matumaini kwa timu yake.
View this post on Instagram
Hata hivyo, mchezo ulivyokuwa ukienda kwenye dakika za mwisho, Zanzibar Heroes walionyesha kiwango cha juu cha ujasiri. Dakika ya 90+5, Hassan Ali Cheda alifunga bao la ushindi kwa Zanzibar Heroes, na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Ushindi huu unaitangaza Zanzibar Heroes kama mabingwa wa Kombe la Mapinduzi 2025, huku wakionesha kiwango cha juu cha soka na ubora wa kiufundi katika michuano hiyo.
Pendekezo La Mhariri: