Hizi Apa Timu Zilizofuzu AFCON 2025
Hizi Apa Timu Zilizofuzu AFCON 2025
Baada ya mitanange ya kukatana shoka baina ya timu za mpira wa miguu za mataifa mbalimbali barani Afrika katika hatua ya makundi ya kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, hatimaye orodha kamili ya timu 24 zilizojihakikishia nafasi imekamilika. Michuano hii mikubwa inatarajiwa kufanyika nchini Morocco, ambayo pia ni mwenyeji wa mashindano haya. Timu ya mwisho kujihakikishia tiketi ni Msumbiji, baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Guinea-Bissau. Katika makala hii, tutakuletea kwa kina orodha ya timu zilizofuzu, matokeo ya kuvutia, na mambo muhimu yaliyoshuhudiwa katika hatua ya kufuzu.
Orodha ya Timu 24 Zilizofuzu AFCON 2025
Ifuatayo ni orodha ya mataifa yaliyofuzu kushiriki mashindano ya AFCON 2025:
- Morocco (Wenyeji)
- Burkina Faso
- Cameroon
- Algeria
- DR Congo
- Senegal
- Misri
- Angola
- Guinea ya Ikweta
- Ivory Coast
- Uganda
- Afrika Kusini
- Gabon
- Tunisia
- Nigeria
- Zambia
- Mali
- Zimbabwe
- Comoro
- Sudan
- Benin
- Tanzania
- Botswana
- Msumbiji
Uchambuzi wa Makundi
- Kundi A: Katika kundi hili, Comoro iliwashangaza wengi kwa kuibuka kileleni kwa pointi 12, ikifuatiwa na Tunisia yenye pointi 10.
- Kundi B: Morocco, timu iliyo na viwango bora zaidi Afrika, iliibuka kidedea kwa alama 18 baada ya kushinda mechi zote za kufuzu, huku Gabon wakifuzu wakiwa na alama 10.
- Kundi D: Nigeria iliongoza kwa alama 11, ikifuatiwa na Benin yenye alama 8, na zote mbili zikijihakikishia tiketi ya kuelekea Morocco.
- Kundi F: Kundi hili lilikuwa na mshangao mkubwa, ambapo Ghana walishindwa kufuzu, huku Angola wakiibuka vinara na alama 14, wakifuatiwa na Sudan yenye alama 8.
- Kundi H: Tanzania na DR Congo walivuka salama kutoka kundi hili, ambapo DR Congo walikusanya alama 12 huku Tanzania wakiwa na alama 10.
Mapendekezo ya Mhariri: