Viingilio Mechi ya Yanga vs Al Hilal 26.11.2024
Viingilio Mechi ya Yanga vs Al Hilal 26.11.2024
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Yanga SC, wametangaza rasmi bei za tiketi za kuingia uwanjani kutazama mchezo wao wa kwanza wa Klabu Bingwa Afrika CAF. Mchezo huo umepangwa kuchezwa Jumanne ya tarehe 26 Novemba 2024 katika Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kuvutia sana kutokana na ubora wa timu hizi mbili, huku mashabiki wa soka Tanzania wakiwa na matumaini makubwa na Yanga SC, klabu ambayo imeonesha kiwango cha hali ya juu tangu kuanza kwa msimu wa 2024/2025. Uongozi wa klabu ya Yanga umeweka wazi viingilio vya mechi hiyo, na hapa chini tunakuletea maelezo yote muhimu.
Viingilio Rasmi vya Mechi
Uongozi wa Yanga SC umetangaza viwango vya tiketi kwa mechi dhidi ya Al Hilal, kuhakikisha kila shabiki ana nafasi ya kuingia uwanjani kulingana na uwezo wake wa kifedha. Hapa kuna viwango vya tiketi kama ilivyotangazwa rasmi:
- Mzunguko (Machungwa): TZS 3,000
- VIP C: TZS 10,000
- VIP B: TZS 20,000
- VIP A: TZS 30,000
Soma pia; Viingilio Mechi ya Simba SC Dhidi ya FC Bravos do Maquis 27/11/2024