Vituo vya Kununua Tiketi Mechi ya Yanga vs Al Hilal 26.11.2024
Vituo vya Kununua Tiketi Mechi ya Yanga vs Al Hilal 26.11.2024
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Yanga SC, wametoa mkeka rasmi wenye orodha kamili ya vituo vilivyothibitishwa kwa ajili ya uuzaji wa tiketi kwa ajili ya mechi yao ya kwanza ya hatua ya makundi ya michuano ya CAF Champions League. Mchezo huu, ambao umepangwa kufanyika Jumanne, tarehe 26 Novemba 2024, katika dimba la Benjamin Mkapa, unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mechi hii inakutanisha Yanga dhidi ya moja ya vigogo wa soka barani Afrika, Al Hilal Omdurman ya Sudan. Mashabiki wa soka wanatarajia mtanange wa hali ya juu kutokana na kiwango bora kilichoonyeshwa na timu zote mbili msimu huu. Ili kuhakikisha kila shabiki anapata nafasi ya kuhudhuria, klabu ya Yanga imetoa orodha ya vituo mbalimbali vya ununuzi wa tiketi jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake.
Hapa chini ni orodha kamili ya vituo vya kununulia tiketi, pamoja na maelezo mengine muhimu:
- Alphan Hinga – Ubungo
- Antonio Service – Sinza, Kivukoni
- Gitano Samwel – Mbagala Zakhem
- Gwambina Lounge – Gwambina
- Jackson Kimambo – Ubungo
- Juma Burrah – Kivukoni
- Juma Burrah – Msimbazi
- Karoshy Pamba – Dar Live (Zakhem)
- Khalfan Mohamed – Ilala
- Lampard Electronics
- Mkaluka Traders – Machinga Complex
- Mtemba Service Co. – Temeke
- New Tech General Traders – Ubungo
- Sabana Business – Mbagala Maji Matitu
- Shirima Shop – Leaders
- Sovereign – Kinondoni Makaburini
- T-Money Ltd – Kigamboni
- Tumpe Kamwela – Kigamboni
- View Blue Skyline – Mikocheni
- Vunja Bei – Dar es Salaam Shops
- Young Africans – Jangwani
Mapendekezo ya Mhariri: